Mustakabali Wa Vijana: Afrika Ya Mashariki

Vijana Wa Afrika MasharikiKuna mambo mengi sana yanayotokea katika jamii yetu,na kila jambo lina sababu yake,na maana yake pindi linapotokea katika maisha yetu.Sisi kama vijana hatuna budi kujifunza katika hayo,tujifunze kutoka makosa ya kiungozi yanayotokea leo hii,tujifunze kutoka makosa ya kiutendaji yanapotokea leo hii,tujifunze kutoka matatizo ya kimaadili yanayozikumba nchi za Afrika ya mashariki na dunia kwa ujumla. Kwa nini natoa wito wa kujifunza katika makosa ya liyofanywa na watu wengine? Jibu pekee ni kutoruhusu matatizo hayo kujitokeze tena katika miaka ijayo, kwani tutakuwa tumepata utashi wa kuyazuia yasitokee au kukabiliana nayo pindi yanapotokea.Vijana tunapaswa kutambua ni sisi ndiyo tunaoamua mustakabali wa maisha yetu.

Yanayotokea leo hii,yana ashiria nini?yana ashiria ya kwamba Afrika Mashariki ipo kwenye mpito(Transion period),kuna mahali tunatoka na kuna mahali tuna kwenda,kuna mabadiliko ya kiuchumi yana yotokea katika nchi zetu za Afrika mashariki,Kuna mabadiliko ya kisiasa na kiungozi yanayotokea,kuna mabadiliko mengi yanatokea,katika hayo mabadiliko hatuna budi kujifunza na kutafakari kwa undani ili tujue nini maana ya mabadiliko hayo,na lipi tufanye kwa ajili ya mustakabali wa maisha yetu yajayo na vizazi vijavyo.

Tunapojifunza na kutafakari tuna kuwa katika nafasi nzuri ya kujipanga kimkakati kwa ajili ya kushughulika na matatizo sugu na masuala muhimu katika maendeleo ya watu wa ukanda wa Afrika mashariki,na tunapo anza kuongelea maendeleo ya watu,tunaongelea elimu yao,afya zao,miundo mbinu wanayotumia kila siku katika shughuli zao za maendeleo.

Sisi vijana leo tunajifunza yapi?Tungejibu vipi swali hilo kama tungeulizwa,au kila mmoja angekuwa na majibu yake?Je tunajua historia ya nchi zetu kabla na baada ya uhuru?Tunafahamu nini kuhusu uchumi wetu?nini haswa tuna itaji katika maisha yetu?

Kama kweli tuna taka uchumi wa nchi zetu ukue na kuwa uchumi imara,hatuna budi kujifunza Zaidi masuala ya uchumi,na kuwa wathubutu kwenye shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali.Tukumbuke mustakabali wa Afrika Mashariki upo kwetu sisi vijana,tunapaswa kujifunza,tunapaswa kuwa wabunifu,na watendaji kwa ajili yetu na maendeleo ya nchi zetu.

Usipo wajibika wewe,nani mwingine awajibike,chukua hatua.Mwaka 2014 tunuie kujifunza na kutenda.